Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu bingwa Tanzania bara Haji Sunday Manara, amethibitisha kupima virusi vya ugonjwa wa Corona na kusema yupo fiti, ila bado hajaridhika anataka kupima tena atakapowasili nchini.

Manara ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kufuatia kuwepo na wasiwasi kama atakuwa na virusi vya ugonjwa huo kwa sababu yupo nje ya nchi kwa muda mrefu na ametembelea nchi kama Hispania, Ufaransa, Canada na Uholanzi.

Manara ameandika: “Wazungu baada ya kunipima Corona wakaniruhusu kupanda ndege yao, kisha kuniletea ubwabwa na mandondo na nikirudi home nitapima tena, bado nitaweka karantini ili nijiridhishe kama nipo fiti” ameandika Manara.

Aidha ameongeza kuandika “Ingawa hadi sasa Alhamdulillah nipo fiti kuliko chuma, ngoja nipige kubwa moja kisha nije kitaani Bongo”

Mkude kukutana na Ndayiragije, ampinga meneja wake
CORONA yasitisha Copa Libertadores, Copa Sudamericana