Msemaji wa Simba, Haji Manara amekamatwa na polisi kufuatia tukio la kupotea kwa mfanyabiashara mkubwa hapa nchini Mo Dewji.

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa Haji Manara tangu jana jioni na kuachiliwa lakini leo tena Oktoba 12, 2018 Manara ameshikiliwa tena na jeshi la polisi kwa kosa la kusambaza taarifa mtandaoni za kupotea kwa Mo Dewji akidai kuwa ametumwa na familia ya Mo.

Aidha kwa taarifa kutoka jeshi la polisi Mo bado hajapatikana na hadi kufikia sasa ametimiza siku moja na masaa kadhaa tangu atekwe na watu wasiojulikana ambao wanadaiwa kuwa ni wazungu wawili.

Mo alitekwa eneo la hoteli ya Colosseum alipokuwa akishuka kwenye gari yake aina ya Range Rover akielekea kufanya mazoezi katika ukumbi unaopatikana kwenye hoteli hiyo.

Watekaji hao walifyatua risasi kadhaa hewani na kumuingiza kwa nguvu kwenye gari yao na kukimbia naye.

Na Mwananchi.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 13, 2018
Dkt. Mpango adai marekebisho ya sheria ya Takwimu hayana tatizo

Comments

comments