Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa ikitokea timu ya Liverpool ikaifunga Manchester United katika mchezo wao wa leo hii wa ligi kuu ya EPL basi ataachana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) nakujiunga na Chama Cha Chauma kinachoongozwa na aliyekuwa mgombea Urais, Hashim Rungwe.

Manara ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.

Timu ya Liverpool inatarajiwa kucheza ugenini katika uwanja wa Old Trafford leo hii kupambana na kikosi cha Jose Mourinho, Manchester United katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.

Liverpool wataingia uwanjani huku wakiwa nyuma ya United kwa alama mbili hivyo kushinda kwao leo kutawafanya kupanda katika nafasi ya pili na kuwapiku mashetani hao wekundu kwakuwa na jumla ya pointi 63 dhidi ya 62.

Kuelekea katika pambano hilo meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema wanahitaji kuwa sawa kwa asilimia 100 ili kushinda mchezo huo.

Wakati kwa upande Mourinho amesema watu wengi wamejaa kutoa mawazo tu juu ya kikosi chake licha ya kuwa ya kwao yanawashinda.

 

 

 

Mamlaka ya Mawasiliano yaifungia redio ya Umoja wa Mataifa
Tillerson asisitiza uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari