Pamoja na kujitahidi na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, Man Utd wameendelea kusota katika uingizaji wa fedha kutokana na biashara inayotegemeza wadau mbali mbali wa soka.

Man Utd msimu uliopita walianguka kimapato kwa kiasi cha paund million 38, baada ya kushindwa kufuzu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hali ambayo ilisababisha michezo yao kupungua pamoja na wadhamini kusita kujiingiza kwenye mchakato wa kibiashara.

Kwa msimu huu mapato kwa ujumla kwenye klabu hiyo ya Old Trafford, ni paund milioni 395.2 ambapo yamekua tofauti na ilivyokua imezoeleka ambapo miaka kadhaa iliyopita hesabu zilionyesha Man utd walikua wakipata kiasi cha paund million 433.2.

Pamoja na fedha za udhamini kuongezeka na na kuvunja rekodi kwa asilimia 14 kwa kufikia pauni milioni 154.9 bado imeonekana klabu hiyo imeshindwa kutimiza kiasi kilichokua kikikusudiwa.

Lakini pamoja kuonekana hivyo, sababu zimetolewa za kueleza kwa nini hali imekua hivyo na mashabiki wametajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kutokana na kususia baadhi ya michezo kwa asilimia 16, hali ambayo iliwakosesha Man utd kiasi cha paund milioni 90.6 huku mapato ya utangazaji yakishuka na kufikia paund milioni 107.7.

Katika mapati ya utangazaji Man Utd imepoteza kiasi cha paund million 28.1.

Sababu nyingine iliyotajwa kuikosesha mapato ya Man Utd, ni kukosekana kwa paund milion 35 ambazo hutolewa klabuni hapo kama sehemu ya gharama ya utangazaji wa michezo yao kupitia televisheni katika michuano ya barani Ulaya ambayo kwa msimu uliopita hawakushiriki.

Neymar da Silva Santos Júnior Atemwa Brazil
Bolt Aikumbuka Shule Iliyompa Elimu