Siku 18 zimepita tangu rapa Nispey Hussle aage dunia kwa kupigwa risasi akiwa dukani kwake The Marathon Clothing Store mjini Loss Angeles Marekani, mashabiki wengi wameibeba kauli kubwa ya  Marathon Continues na wengi kuahidi kuitekeleza.

Kauli hiyo ilianzishwa mara tu baada ya kifo chake huku wasanii wakubwa nchini humu akiwemo TI ambae alinunua vitu vya thamani dukani hapo kama heshima ya kukiendeleza alichokiacha Nispey.

Hata hivyo mitandao mingi nchini Marekani imeripoti kuwa duka la nguo la TheMarathon Clothing store limepokea oda za nguo mtandaoni zenye thamani ya  dola za Kimarekani milioni 2 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 4 za Kitanzania kwa muda mfupi tokea Nipsey Hussle afariki dunia.

Rapper Nispey Hussle alipumzishwa April 12,2019 katika makaburi ya Forest Lawn Memorial Park yaliyopo Hollywood Hill na mpaka sasa mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji hayo ameshafikishwa Mahakamani na kufunguliwa shtaka la mauaji.

Kodak black achafua hali ya hewa kwa mashabiki, Polisi waingilia kati
Sugu agoma kusoma hotuba ya upinzani bungeni

Comments

comments