Kamanda wa jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa ametoa taarifa kuwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa sasa siyo mtuhumiwa hadi pale uchunguzi utakapokamilika.

Hidi kufikia leo Mei 8, 2019, Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kwa kushirikiana na mkurugenzi wa makosa ya jinai (DIC) wameanza uchugunzi wa video ya ngono inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidhaniwa kuwa ni ya askofu Gwajima.

“Jeshi la polisi kanda maalum limeanza uchunguzi wa video hiyo mara moja na linapenda kuwapa wananchi taarifa kuwa Gwajima siyo mtuhumiwa, ni muathirika wa tukio hilo kwani tukio hilo linaweza kufanywa na mtu yeyote kwa njia ya kutaka kuharibu heshima yake” amesema kamanda Mambosasa.

Hata hivyo jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuacha kusambaza video hiyo kwakuwa ni kosa la jinai na limewataka waumini wa kanisa hilo kuwa watulivu kwani uchunguzi unaendelea ili kubaini aliyesambaza na lengo lake.

 

 

Serikali kuendelea kutoa elimu bora ya Kilimo
Mke wa Askofu Gwajima atoa neno sakata la video chafu