Siku nne baada ya ndege ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka jijini Addis Ababa kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya kuanguka ikiwa na watu 157, mengi yameibuliwa.

Tumekuandalia mambo sita muhimu unayopaswa kuyafahamu hadi sasa kuhusu ndege hiyo iliyokuwa na miezi minne tu tangu inunuliwe.

  1. Muda wa kuanguka

Ndege hiyo ilianguka dakika sita tu baada ya kuruka kutoka jijini Addis Ababa ikielekea jijini Nairobi nchini Kenya. Iliondoka uwanjani hapo majira ya saa mbili na dakika 38 asubuhi, kwa saa za Ethiopia. Saa mbili na dakika 44 ilianguka katika eneo la Turu Fara, karibu na mji wa Bishoftu.

  1. Tatizo la kasi ya kuruka

Ingawa chanzo halisi cha janga hilo hakijafahamika, taarifa zilizotolewa na rubani wa ndege hiyo, Yared Getachew ambaye Shirika la Ndege la Ethiopia limedai kuwa alikuwa na uwezo mkubwa wa kikazi, ujuzi na uzoefu alieleza kuwa anapata shida katika kuruka kwenda juu (wima).

Rubani huyo aliomba kurejea katika eneo hilo akidai kuwa ingawa anaweza kuona vizuri, kuna shida katika urukaji. ‘Flightradar24’ imeripoti kuwa kasi ya ndege hiyo kuruka kwenda juu (wima) haikuwa imara. Kisha, ilipoteza mawasiliano.

  1. Mfanano wa tatizo na ndege nyingine ya Boeing iliyoua watu 189

Uchunguzi uliofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) ikishirikiana na Bodi ya Ufaririshaji ya Ethiopia, umeonesha kuwepo kwa mfanano vithibitisho/vielelezo walivyovipata kwenye ndege hii ya Ethiopia na Boeing 737 ya Indonesia iliyoanguka Oktoba 29 mwaka jana na kuuawa watu 189.

“Uthibitisho tulioupata kwenye eneo la tukio vinafanana zaidi na sababu za kuanguka kwa ndege ya Indonesia,” Dan Elwell, Kaimu Mtawala wa FAA anakaririwa na Reuters.

Kisanduku cheusi cha kutunza kumbukumbu ya mwenendo wa ndege kimepelekwa nchini Paris kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Boeing 737 iliyokuwa inamilikiwa na Shirika la Ndege la Lion Air ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa jiji la Jakarta nchini Indonesia.

The Boeing 737, owned by the low-cost airline Lion Air, went down after taking off from the capital Jakarta.

 

  1. Boeing waliwahi kutoa maelekezo mapya ya kutumia program ya kompyuta kwenye ndege zao

Baada ya ndege ya Indonesia kuanguka, Boeing waliwahi kutoa muongozo mpya kwa ajili ya kuwasaidia marubani wake kutumia kifaa maalum cha ndege kinachodhibitiwa na mfumo wa kompyuta kitwacho Manoeuvring Characteristics Augmentation System (MCAS). Kifaa hicho kinasaidia ndege kutoongeza mwendo inapopanda juu kwa kona kali ya wima.

  1. Upya wa kifaa maalum kwenye Boeing 737

Boeing 737 imefungiwa kifaa kipya kutengenezwa na shirika hilo, ambacho ni sawa na MCAS. Ingawa Boeing wameeleza kuwa wana uhakika na ubora wa kifaa hicho kilichozaa jina la kitaalam Max, imeamua kusimamisha utendaji kazi wa ndege zake zote. Ndege iliyoanguka ni Max8. Hadi mwaka 2017, Boeing walikuwa wameshatoa toleo jipya la Max8 kwa ndege 350. Matoleo mengine mapya yanayoitwa Max7 na 10 bado yanaandaliwa na yanatarajiwa kuingia sokoni miaka michache ijayo.

Kifaa hiki ndicho kinachoaminika kuwa kinaweza kuwa ni chanzo cha kuwachanganya marubani wanapokutana na tatizo, kwani inadaiwa kuwa badala ya kuipeleka ndege husika kwenye eneo la bahari na kutua kwa namna fulani inapobaini tatizo ‘automatically’, kinaweza kuwa kiliwachanganya marubani na kukata mawasiliano. Hata hivyo, Boeing wameendelea kushikilia msimamo wao kuwa wanakiamini kifaa hicho na yasemwayo hayana ukweli.

  1. Nchi zilizositisha safari za ndege za Boeing 737

Nchi kadhaa zimesitisha matumizi ya safari, lakini kwa sasa Marekani, Brazil, Uingereza, China, Australia na India.

Kati ya ndege 350 zenye modeli ya Max8, ndege nyingi zaidi zinamilikiwa na nchi za Marekani, Canada na China.

Hali hii ni pigo kubwa kwa Shirika hilo la ndege, kwani aina hii ya Boeing 737 Max ilikuwa imeweka historia ya mafanikio. Ilikuwa imepewa oda 4500 na wateja takribani 100 duniani kote.

Boeing 737 Max8 ilikuwa moja kati ya ndege 30 za aina hiyo zilizokuwa zimeagizwa na Serikali ya Ethiopia kama sehemu ya juhudi ya kutanua wigo wa Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines).

7. Historia ya ajali za ndege za Shirika la Ndege la Ethiopia

Hadi Machi 2019, Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Ethiopia imeweka kumbukumbu ya ajali 64 za ndege za Shirika la Ndege la Ethiopia ambazo zimesababisha jumla ya vifo vya watu 459 tangu mwaka 1965, na pia ajali nyingine sita zilizotokea wakati wa shirika la zamani la ndege la nchi hiyo.

*Taarifa hii imetokana na taarifa zilizokusanywa kupitia Mashirika mbalimbali ya habari kama Reuters, BBC, na CNN.

Mtangazaji apigwa vibaya na aliojaribu kuwasaidia katika ajali
Makamu wa Rais akutana na Watanzania waishio Uganda