Kiafya haishauriwi kufanya vitu vifuatavyo mara baada ya kula chakula hasa namba nne ni hatari zaidi kwa maisha yako, Kawaida mara baada ya kula chakula hasa cha usiku mtu hupendelea kujilaza au kukaa kwenye kiti, hii inatajwa kuwa ni kosa kubwa ambalo hutakiwi kulifanya mara baada ya kula, Kwa mujibu wa wataalamu wanasema kuwa kitendo hiko ni hatari sana na kinaweza kuweka afya yako katika hatari kubwa.

  1. Kuvuta sigara

Kiafya mara baada ya kula chakula hairuhusiwi kuvuta sigara japo kuwa mvutaji wa siagara hupatwa na hamu kubwa  ya kuvuta mara baada ya kula tabia hii huhatarisha afya, hivyo inashauriwa kusubiri angalau kwa masaa kadhaa ndipo uvute endapo ni lazima sana kwani sigara ina miliki Nikotini kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, madhara yanayotokea kwa kuvuta sigara mara baada ya kula chakula ni sawa na madhara yanayotokea kwa mtu aliyevuta sigara 10  kwa mara moja na hii huchangia mtu kupata kansa ya mapafu.

2. Kula matunda

Wanasayansi wamedhihirisha kuwa kiafya matunda yanatakiwa kuliwa kabla ya kula si mara baada ya kula kama ambavyo imezoeleka kwa watu wengi, Matunda yana enzymes na asali asili ambayo inahitaji kumeng’enywa ndani ya muda wa kutosha, hivyo kula matunda baada ya chakula inaweza kusababisha matatizo ya mmeng’enyo wa chakula pamoja na kiungulia.

3. kulala

Kulala mara baada ya kula ni kitendo ambacho hupendelewa kufanywa na mamilioni ya watu japokuwa tabia hii si nzuri kiafya, kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wansayansi wa chuo kikuu cha Loannina Medical watu wanaosubiri kulala kwa kitambo kidogo mara baada ya kula wana nafasi ndogo ya kupata ugonjwa wa mshtuko na hii ndio sababu inashauriwa kukaa masaa mawili mara baada ya kula ndipo kulala.

4. kuoga

Kuoga mara baada ya kula ni moja ya kitu kibaya na hatari sana kwani kwa kufanya hivyo  unaweza kudhuru afya yako, Kuoga maji ya moto kunasababisha kuongeza kasi ya mzunguko wa damu kwenye miguu na kupunguza kasi ya mzunguko wa damu tumboni kitu ambacho kina madhara kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

5. Kunywa Chai

Chai ni afya lakini haitakiwi kutumiwa mara baada ya kula chakula, Kunywa chai baada ya kula inaweza kuingilia ufyonzaji wa madini wa chuma katika mwili wako kwani chai humiliki asidi  aina ya Tannic ambayo inakusanya pamoja madini ya chuma na protini kwenye chakula, matokeo yake ni kwamba 87% ya madini ya chuma hupungua kwa kiasi kikubwa hali inayopelekea mtu kukumbwa na magonjwa kama Anemia, kizunguzungu na kuchoka kutokana na kukosa madini ya chua mwilini.

Harry Maguire, Jerome Boateng waigawa Man Utd
Mwanasiasa wa upinzani kutoka Zimbabwe anyimwa hifadhi Zambia