Mamba amesababisha taharuki katika hospitali ya mji wenye migodi ya dhahabu wa Hwange nchini Zimbabwe.

Ripoti za vyombo vya habari nchini humo vimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne jioni wiki hii ambapo dereva wa taxi alikuwa wa kwanza kumuona mamba huyo na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama.

“Ndani ya dakika tano nilipokea takribani simu 10 za wakaazi wa eneo hilo waliokuwa kwenye taharuki kubwa,” Afisa mwandamizi wa bodi ya makaazi, Themba Tshuma anakaririwa.

“Mengi yamezungumzwa na wakaazi wa eneo hilo waliokuwa hawaamini wanachokiona. Wengine wamehusisha na ushirikana, wamedai kuwa inawezekana alikuwa ni mtu mshirikina ambaye alishindwa kufuata masharti na kujikuta anageuka kuwa mamba,” aliongeza.

Gazeti la The Chronicle limeeleza kuwa mamba huyo alikaa katika geti la hospitali hiyo na kutishia kumshambulia mtu yeyote aliyesogelea geti. Hata hivyo, maafisa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Zimbabwe walifika na kumuua mamba huyo.

Haijafahamika rasmi alikotokea mamba huyo kwani chanzo kikubwa cha maji kiko umbali wa kilometa kumi kutoka kwenye mji huo.

Maradona amtetea Messi
Kamanda aahidi ukilema kwa watakaoandamana Aprili 26