Mwanamke mmoja mkazi wa kaunti ya Nakuru nchini Kenya  amempa adhabu ya kumshona mdomo mtoto wake wa kiume anayesoma darasa la tano kwa kosa la kushuka kimasomo.

Kwamujibu wa gazeti la Daily Nation la nchini humo tukio lililofanywa na mama huyo liliwaacha wakazi wa eneo hilo na bumbuwazi kwa kuto kuamini kilichotokea.

Jirani yake mmoja  amesema kuwa mwanamke anayefanya kazi kwenye saluni ya urembo aliumizwa na maendeleo ya mtoto wake shuleni yaliyokuwa yameshuka, hivyo katika kumuadhibu mama huyo alimshona mdomo mtoto wake kwa kutumia sindano kabla ya majirani kuingilia kati.

Kamishna msaidizi wa kaunti hiyo, Julius Nyaga ameiambia Daily Nation kuwa taarifa za tukio hilo zimefika na polisi bado wanamtafuta mama huyo kwani tukio hilo ni lakikatili na sheria itafuata mkondo wake.

“Polisi wanamtafuta mama wa mtoto baada ya uongozi wa shule kuripoti kwenye mamlaka” ameeleza kamishna msaidizi Nyanga.

Na kuwataka wazazi kuacha kuwafanyia vitendo vya kikatili watoto kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria na kuwashauri kuwa ni vyema kwa wazazi kutafuta msaada wa kitaalamu kuwasaidia watoto badala ya kuchukua hatua kali zinazosukumwa na hasira.

 

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 7, 2019
Muuguzi aliyeuwa wagonjwa 85 afungwa maisha

Comments

comments