Mkazi wa kijiji cha Ndachi mkoani Dodoma Bi Asha Juma anashutumiwa kwa kosa la kumchoma mwanae mikono kwa maji ya moto kwa kile kilichoelezwa ni udokozi wa nyama.

Kaimu mganga mkuu kitengo cha upasuaji hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma Dkt. Kato Peleusdr amethibitisha kumpokea Godfrey Banda mwenye umri wa miaka 13 hospitalini hapo.

Awali mashuhuda wa tukio hilo wameelezea namna mama huyo alivyomtendea mwanae kitendo hicho cha kikatli.

Bi. Joyce Julias ambaye ni mwenyekiti wa ndachi kata ya mnadani ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa serikali pindi wanapoona matukio ya kikatili katika jamii.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Vedastus Matagy kutoka Hospital ya general amesema kuwa Jamii kutokuwa na utayari wa kuripoti matukio ya kikatili na unyanyasaji ndiyo sababu ya kuongezeka kwa vitendo hivyo.

Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inatamka wajibu wa jamii katika kumlinda na kutunza haki za mtoto ili kuhakikisha analelewa na kuwa ustawi mzuri katika maisha yake ,lakini bado haki za mtoto zinavunjwa.

 

Kocha wa Cameroon aliyetekwa aachiwa, klabu yaeleza kulikoni
Kimbunga Idai chaleta maafa, magari ya misaada yakwama

Comments

comments