Mali za mpinzani wa rais wa Rwanda, Paul Kagame zimepigwa mnada mara baada ya mamlaka ya ukusanyaji wa kodi nchini humo kuzizuia ikidai kuwa zinadaiwa kodi ya kiasi cha dola milioni 7.

Diane Rwigara ambaye yuko kizuizini alizuiwa kuwania urais mwaka uliopita na baadaye kukamatwa kwa madai ya uchochezi na kutaka kufanya mapinduzi ya serikali.

Halmashauri ya ukusanyaji mapato nchini Rwanda imeuza mashine za kuchakata tumbaku kwa takriban dola milioni 2 katika hatua ya kulipia kodi inayodaiwa familia hiyo ambayo inaripotiwa kudaiwa dola milioni 7.

Aidha, familia hiyo ya mwanasiasa mkosoaji wa rais Kagame imesema kuwa hatua hiyo ya kuuza mali na mashtaka dhidi yake imechochewa kisiasa.

Mauzo ya awali ya biashara za familia ya Rwigara ya tumbaku yaliingiza dola milioni 595, ambapo Rwigara ambaye ni mtetezi maarufu wa haki za wanawake nchini humo na familia yake, wamesema kuwa matatizo yake yalianza wakati alipoamua kugombea urais.

Hata hivyo, Rigwara alikamatwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara Septemba 2017 nyumbani kwake kwenye mji mkuu Kigali.

Salah awafikirisha kocha na kipa wa Urusi, ‘tutaona’
Rapa wa Marekani auawa kwa risasi, aacha rekodi nzito