Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  amesema atakutana na kina mama wajane, jijini Dar es Salaam, Aprili, 4,  mwaka huu, ili kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili.

Likiwemo suala la mirathi  na kutoa elimu kwao kuhusu fedha ambazo ni asilimia nne zinazotengwa kila manispaa kwa wanawake ili wajue kuwa fedha hizo zinawahusu.

”Wajane wengi wanateseka na mirathi na ndani ya mirathi wapo ambao tayari hukumu zimetoka… wapo wengine ambao wanshindwa pesa za kuwalipa sheria wapo wengine wanashindwa hata waende wapi ili waweze kupata haki zao walichuma pamoja wameteseka pamoja lakini wamebaki wakilea watoto bila mahali na wengine wamekuwa wakifukuzwa hata kwenye nyumba walizochuma na waume zao” Amesema Makonda.

Makonda ameyasema hayo ofisini kwake leo akiongea na waandishi wa habari.

Pia amepongeza wakuu wa wilaya za Ilala na Temeke kwa kukamilisha zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo-wadogo kwenye maeneo yao.

Aidha amewataka wakuu wa wilaya za Kigamboni, Kinondoni na Ubungo kuongeza kasi ya kukamilisha zoezi hilo.

 

LIVE : Rais Magufuli akifungua kiwanda cha kubangua Korosho Mtwara
Rais wa Algeria atangaza tarehe ya kujiuzulu

Comments

comments