Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kuwasiliana na viongozi wa usalama wa Taifa ili kuiombea Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni jengo lililoachwa na Hayati Aboud Jumbe ili walitumie kama Ofisi.

Makonda amesema hayo leo Novemba 19, 2016 wakati akijibu changamoto zilizotolewa na mkuu wa wilaya hiyo, Hashimu Mgandilwa ambaye amemuomba Makonda kuwaombea eneo la Ofisi za Wilaya kwani kwasasa wanaofisi nane katika maeneo tofauti, hivyo wamemuomba kuwaombea nyumba iliyoachwa na Hayati Aboud Jumbe iliyokuwa inatumiwa na watu wa usalama wa Taifa.

Aidha, Makonda amesisitiza uwajibikaji wa kila mtendaji wa Serikali kwani kila mtumishi akiwajibika kwa nafasi yake yatafikiwa malengo ya kupatikana Dar es salaam mpya yenye tija kwa Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Makonda amemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Kigamboni, Steven Katemba kuhakikisha watendaji wanasikiliza kero za wananchi na kutoa ripoti kila wiki ya kero zilizosikilizwa.

 

Muhongo agonga mwamba tanesco, bei ya umeme kupanda kama kawaida
#HapoKale