Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wazazi na walezi kuchunguza mienendo ya tabia za watoto wao ili wasije wakajihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kujiunga na vikundi vya uhalifu kama Panya Road.

Ameyasema hayo katika muendelezo wa ziara yake ya siku kumi ya kuutembelea mkoa wa Dar es salaam na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, amesema wazazi wana wajibu mkubwa sana wa kuwachunguza watoto wao ili kuweza kujua wanajihusisha na kitu gani.

Aidha, Makonda  amewataka wanafunzi wa shule ya msingi Mbande, kuwa wasikivu kwa Wazazi wao, Walimu, Viongozi wa dini na watu wote ili waweze kutimiza malengo na wajitahidi kusoma kwa bidii kwani kufanya hivyo ni kumuunga mkono, Rais John Pombe Magufuli, katika adhima yake ya kuboresha elimu.

Katika hatua nyingine, Makonda amezindua madarasa matatu katika shule ya msingi Mbande iliyoko mbagala wilaya ya Temeke, yaliyojengwa kwa ufadhili wa Rais Magufuli.

Hata hivyo ameongeza kuwa wazazi au walezi wanatakiwa kuwasimamia vyema watoto wao ili kuwalea na kuwajenga katika maadili mema ambayo yatasaidia taifa kuwa na watu wenye weledi na wachapakazi.

#HapoKale
Shaka: Ukiona unanyanyaswa ndani ya ccm, milango iko wazi