Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amepiga marufuku baadhi ya watendaji wanaozuia wasanii kurekodi video za nyimbo au muvi kwenye mandhari mbalimbali za jiji hilo na kusema kuwa kufanya hivyo kunairudisha nyuma sekta ya utalii.

Kufuatia onyo hilo, Makondoa amehalalisha maeneo mbalimbali na kutoa kibali kwa wasanii kufanya kazi zao katika maeneo mbalimbali isipokuwa Ikulu, Mahakama, maeneo ya jeshi na vituo vya polisi ambapo panahitaji vibali maalumu

”Haiwezekani akitaka kurekodi video au muvi kwenye mitaro ya maji machafu ambayo inatoa taswira mbaya kwa jiji letu haisumbuwi vibali lakini akirekodi kwenye hoteli, Majengo marefu, fukwe au kwenye mazingira mazuri anasumbuliwa kibali hili haliwezekani,

”kuanzia sasa wasanii mtarekodi video location yeyote mnayotaka isipokuwa Ikulu, Mahakama, maeneo ya jeshi na vitupo vya polisi ambapo panahitaji vibali maalumu” Makonda.

Makonda amesema lengo likiwa ni kuwapa fursa wasanii kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo jijini kupitia kazi ya sanaa.

“leo hii Ikulu ya Marekani ‘White House’ inajulikana kutokana na muvi zao wengine hatujawahi kutembelea baadhi ya nchini lakini ukiangalia ‘movie’ unaambiwa ndio sehemu fulani unakubali kumbe hata wakati mwingine unadanganywa’. Amesema Makonda.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema inapaswa ifike wakati wasanii waliopo nchini Tanzania hasa katika jiji lake wawe wanarekodi kazi kwa uhuru bila ya kupatiwa shida ya aina yeyote ile.

Mugabe atoa dukuduku baada ya kung'olewa madarakani
Bunge lampitisha Xi Jinping kuongoza bila kikomo