Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anaendelea na ziara yake mkoani humo ambapo leo ameianza wilaya ya Kinondoni, huku akiwaogusa watumishi wa umma aliodai wanatumia hirizi.

Akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya hiyo, Makonda alisema kuwa anafahamu wapo wanaoshinda kwa waganga na wanaotumia hirizi ili kujikinga wasitumbuliwe.

“Kuna baadhi ya watumishi wanatembea na hirizi ili wasitumbuliwe, wakikutana na viongozi wao wanazibinya,” alisema Makonda. “Mimi ninachokitaka kutoka kwenu ni kuwatumikia wananchi wa chini,” aliongeza.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Ally Hapi aliwaambia watumishi hao kuwa atahakikisha anawashughulikia watendaji ambao hawawajibiki ipasavyo katika kuwaletea maendeleo wananchi wao

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam anaendelea na ziara yake katika wilaya za mkoa huo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mzimu Wa Majeraha Wamuandama Mathieu Debuchy
#HapoKale