Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, ameahidi kutoa pesa kiasi cha milioni 5 ili kumsaidia mama mzazi wa msanii Godzilla, kuendeleza biashara aliyokusudia kuianzisha.

Ameyasema hayo wakati akizungumza mbele ya waombolezaji waliofika kutoa heshima zao za mwisho kwa Godzilla, ambapo amesema kuwa aliambiwa kuwa marehemu alikuwa na ndoto kubwa ya kumsaidia mama yake kiuchumi na kumpa kiasi cha pesa ili afungue duka la madawa, lakini alitumia pesa hiyo kumuuguza alipokuwa akiumwa.

“Nimeambiwa kuwa marehemu alikuwa na ndoto kubwa ya kumsaidia kiuchumi mama yake, na alitoa kiasi cha pesa ili afungue duka la madawa, lakini pesa hiyo ilitumika katika kumuuguza Godzilla, hivyo mimi nitatoa milioni tano siku ya Jumatano, ili kumsaidia mama kiuchumi na kumsaidia kutunza wajukuu alioachiwa”, amesema Paul Makonda.

Ikumbukwe kwamba Godzilla ndiye alikuwa tegemeo kubwa kwa familia yake, hivyo kifo chake kimeipa wakati mgumu zaidi.

Hatufundishi askari wetu kuua watu- Kangi Lugola
Viongozi wa Dini nchini waaswa kuliombea Taifa na Rais Magufuli

Comments

comments