Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ambaye alipiga marufuku shughuli zote za ibada zinazofanyika katikati ya juma kwenye wilaya yake na kuwataka kuzitumia siku hizo kufanya kazi.

Hivyo Mjema aliagiza ibada zote kufanyika siku zilizoelekezwa ambazo ni Ijumaa kwa waislamu, Jumamosi kwa wasabato na Jumapili kwa wakristu wengine, na kudai kuwa kikundi chochote cha kidini kitakachofanya ibada nje ya siku hizo kitachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili.

Hata hivyo Makonda ameenda kinyuma na kauli hiyo na kuwataka wananchi wa Ilala kuabudu na kuendelee kufanya ibada kama kawaida.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumanne ya Oktoba 22, 2019 baada ya kuulizwa na wananchi katika mkutano na waandishi na wahabari kuhusu kauli hiyo ya Sophia Mjema ya kufuta Ibada katikati ya wiki.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii Mjema alisikika akisema.

”Siku nyingine wananchi wa Ilala wanatakiwa kufanya kazi, Tunajua kwenye kumuomba Mungu ni mara tatu, yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili siku nyingine ni marufuku, nyinyi kazi mnafanya saa ngapi?”.

 

Twiga Stars yajiandaa kutetea ubingwa wa CECAFA
Zimbabwe: Tembo 55 wafa kwa kukosa maji ya kunywa