Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema mwaka 2012 alipewa nauli na Rais Mstaafu Benjamini Mkapa kwenda Dodoma kugombea makamu mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM)

Amesema hayo leo katika uzinduzi wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mfuko wa maendeleo ya jamii (Tasaf) Jijini Dar es Salaam ambapo amesema naye amenufaika na mfuko huo kwa sababu alipewa nauli na Rais Mkapa ambaye ni mwanzilishi wa mfuko huo.

”Namshukuru sana Rais Mkapa kuona bado anaendelea kufanya kazi yake naomba Rais Magufuli niseme mbele yako mfuko huu wa Tasaf nami  nimenufaika nao haikuwa moja kwa moja” amesema Makonda

Hata hivyo amesema kuwa wananchi kutoka mitaa 304 ya mkoa wa Dar es Salaam wamenufaika na mfuko huo.

”Wengi wamekuwa waamifu kutumia kama maelekezo yalivyo fedha hiyo imetumika kama mbegu na inatumika kuongeza chachu ya maendeleo kwa mtu mmoja, familia na Taifa” amesema Makonda

Rapa 50 Cent amkana French Montana
Trilioni 1.4 zatumiwa na Tasaf kunusu kaya maskini

Comments

comments