Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo Julai 12, 2018 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya Mwenge huo kukamilisha shughuli ya uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 32.

Makonda amesema kuwa ndani ya siku tano ambazo mwenge ulikuwa jijini Dar es salaam umefanikiwa kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 36 ya maendeleo kwenye wilaya zote tano.

Aidha, Makonda amewashukuru wananchi wa Dar es salaam kwa ushirikiano mkubwa walioonyesha tangu siku mwenge ulipoingia hadi leo alipoukabidhi kwa mkoa wa Pwani.


EXCLUSIVE: Uhamiaji wataja mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu ‘PASSPORT’

Waziri Mkuu awataka viongozi wa dini kuwekeza kwenye viwanda
Majaliwa aagiza maafisa ugani kuwezeshwa na kusimamiwa kikamilifu

Comments

comments