Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameibua madudu katika miradi mbali mbali  ya uboreshaji wa Miundo mbinu ya Mkoa wa Dar es salaam DMDP ambayo ilitakiwa kulipwa kwa watu ambao ni hewa.

Ameyasema hayo mapema hii leo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa  habari, amesema kuwa kuna zaidi ya Shilingi bilioni tano na milioni mia saba hazikustahili kulipwa.

Aidha, Makonda amesema makampuni yaliyopewa kuthamini ardhi hayana sifa za kufanya kazi hiyo na kuongeza kuwa kuna watu ambao walijipanga kuiibia Serikali bilioni sabini hivyo udanganyifu huo haukubaliki.

“Nimeiagiza takukuru kufanya uchunguzi ili watuhumiwa wote waliohusika ndani ya wiki wawe wamepelekwa mahakamani mara moja,”amesema Makonda.

Hata hivyo,  Makonda amesema kuwa wizi huo haukubariki kwani kufanya hivyo ni kuiibia Serikali na kujirudisha nyuma kimaendeleo

 

LIVE BUNGENI: Yanayojiri Uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki
TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya kodi

Comments

comments