Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika wiki ya asasi za kiraia nchini (AZAKI) itakayofanyika jijini Dodoma Novemba 4 hadi 8, 2019 ikiwa na kauli mbiu isemayo “ubia kwa maendeleo, ushirikiano kama chachu ya maendeleo”

Akizungumza Jijini Dodoma hii leo Oktoba 31, 2019 Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya foundation for civil society (FCS) Francis Kiwanga amesema katika wiki hiyo asasi za kiraia zaidi ya 500 zitakutana kutoka Tanzania bara na visiwani.

Amesema wiki hiyo itaambatana na maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na asasi hizo kwa lengo kuimarisha ubia baina yao na wadau mbalimbali katika kusongesha mbele gurudumu la maendeleo na kuinua uchumi wa Taifa.

“Katika wiki hiyo kutakuwa na maoneaho mbalimbali ya kazi za wadau maana lengo la kongamano hilo nikuimarisha ubia kati ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika juhudi za kujiinua kichumi na maendeleo kwa Taifa,” amefafanua Kiwanga.

Amesema kupitia kongamano hilo watafanya majadilianao juu ya kazi zao, kubadilishana uzoefu na kuona ni jinsi gani wanaweza kushirikiana na wananchi, serikali, bunge, wabia wa Maendeleo na sekta binafsi.

Awali akiongea katika mkutano huo Mbunge wa viti maalumu wa mkoa wa Dodoma Fatma Tawfiq amewataka wananchi kuhudhuria maonesho hayo ili kufahamu shughuli na umuhimu wa asasi hizo kwa maendeleo ya jamii.

Amesema jamii inapaswa kufahamu kuwa asasi za kiraia si adui wa serikali na badala yake washirikiane nazo katika kujiletea maendeleo ya pamoja kiuchumi na huduma mbalimbali kwa wananchi.

“Ipo dhana kwamba asasi za kiraia hupokea fedha kutoka kwa wafadhili na kuzitumia isivyo kitu ambacho si cha kweli kwani ubadhirifu wa fedha ni hulka ya mtu binafsi,” amesisitiza Mbunge Tawfiq.

Kwa upande wake mwakilishi wa Msajili wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOS), Charles Komba amesema serikali inatambua umuhimu wa asasi za kiraia kwani zimesaidia kufikisha huduma katika maeneo ambayo ni nadra kwa kuyafikia.

Naye afisa uhusiano wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Michael Malya amesema katika wiki hiyo kituo hicho kitakuwepo na kitajihusisha na utoaji wa huduma za kisheria.

Uaandaaji wa wiki ya AZAKI unaratibiwa na zaidi ua asasi za kiraia 15 ambazo ni FCS, LHRC, LSF, Save the children, Wajibu Institute, UN Women, Oxfam, Twaweza, Policy Forum, msichana Initiative, haki rasilimali, UNA Tanzania, Acountability Tanzania, Sikika, TLS, SHIVYAWATA na TANGO.

Polisi wapekua nyumbani kwa Idriss
Takukuru kumfikisha Kigogo wa serikali Mahakamani