Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza kukamatwa kwa wazazi wenye tamaa ya fedha ambao wamekuwa wakiwakatisha masomo mabinti zao kwa ajili ya kuwaozesha.

Ametoa agizo hilo Wilayani Uyui Mkoani Tabora  katika mkutano wa hadhara, ambapo amesema kuwa kuanzia sasa Watendaji wanatakiwa kuwakata na kuwafikisha katika vyombo vya dola bila woga wazazi wa binti na wale wa kijana wanakatisha masomo ya watoto wa kike kwa lengo la kuwaozesha.

“Nawaagiza Watendaji wote kuwakata wazazi wa binti na wale kijana ambao mtawakuta wakiwa wanawaozesha mabinti wao ambao kimsingi walipaswa kuwa shule……msimuogope mtu wakamateni wote wawe wazazi wa binti hata wa yule anayetarajia kuoa ili hatua kali za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa,”amesema Majaliwa.

Aidha, amewaonya pia vijana ambao wanamiliki na kuendesha pikipiki maarufu kama boda boda ambao wamekuwa wakiwapakia wanafunzi kwa lengo la kuwarubuni ili wajihusishe na vitendo vya ngono kuacha mara moja.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mtu atakayekamatwa Serikali itamfikisha Mahakamani ili aweze kupata adhabu kali.

 

Sumaye: CCM wananifanyia fitina kuninyang'anya mashamba
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 13, 2017