Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea wanachama wapya 60 kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

 Wanachama hao wamepokelewa leo mchana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Nkowe kata ya Nkowe, wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

 Aidha, kabla ya kuwakabidhi kadi za CCM, Majaliwa alipokea kadi za CUF kutoka kwa vijana saba kwa niaba ya wenzao 60.

 Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Barnabas Essau amesema kuwa wanachama wote ni vijana ambao wanajishughulisha na shughuli mbalimbali na wameridhishwa na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano.

 Hata hivyo, Novemba 5, mwaka huu, Waziri Mkuu alipokea wanachama 37 kutoka vyama vya CUF na CHADEMA kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mbekenyera, wilayani Ruangwa.

Dkt. Mpango: Deni la taifa ni himilivu
Wanaume wanunua machangudoa sasa kutiwa mbaroni