Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa siku 16 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Magreth John awe amepeleka asilimia 20 sawa na shil. milioni 114 ya kijiji cha Holili kabla ya machi 10 mwaka huu, fedha hizo zinatokana na mauzo ya madini aina ya pozolana.

Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na watumishi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Holili pamoja na wananchi wa kijiji cha Holili, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro.

Majaliwa ametoa maagizo hayo baada ya wananchi wa kijiji cha Holili kuwasilisha malalamiko yao kupitia mabango wakimuomba awasaidie ili Halmashauri hiyo iweze kulipa fedha zao zinazotokana na mapato ya mauzo ya madini hayo yanayochimbwa kijijini kwao.

“Mkuu wa wilaya (Agness Hokororo) simamia kuhakikisha kiasi hicho cha fedha kinakwenda kwa wananchi na Mkuu wa Mkoa (Dkt. Anna Mgwira) nataka nipate taarifa kuwa fedha hizo zimeshalipwa kwa uongozi wa kijiji husika.”amesema Majaliwa

Aidha, Majaliwa amewataka watendaji katika maeneo mbalimbali nchini kuwa wamepelekwa huko kwa ajili ya kuwahudumia wananchi, hivyo hawana budi kutenga muda wa siku tatu kwa wiki na kwenda maeneo ya vijijini kusikiliza kero zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Pia amesema kuwa hali ulinzi na usalama katika mpaka huo si nzuri, hivyo serikali imeamua kuimarisha ulinzi kwenye mpaka huo, ni muhimu kwa wananchi washirikiane katika kuulinda mpaka huo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wote watakaokamatwa wakipita au kuingiza mizigo kupitia njia zisizo rasmi kwa sababu hao ndio wanaopitisha silaha.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wananchi wa Tanzania na Kenya hawajazuiwa kufanya biashara upande wowote bali wanatakiwa wafuate sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika nchi husika ikiwa ni pamoja na kutumia njia rasmi.

 

 

Halmashauri zote nchini zatakiwa kutenga 10% ya mapato
Familia moja yahukumiwa kwenda jela miaka 30 Mpwapwa