Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amechukizwa na vitendo vya watoto wa kike kukatisha masomo yao kwa kupata ujauzito wilayani Nyang’hwale ambapo jumla ya wanafunzi 72 wamepata ujauzo katika kipindi cha miaka mitatu cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2018.

Majaliwa amesema hayo akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba, ,kijiji cha Kalumwawilaya ya Nyang’hwale, akiwa katika ziara yake mkoani Geita.

Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa wilaya hiyo, Hamim Gwiyama kufanya operesheni katika kila kijiji na kubaini waliowapa wanafunzi ujauzito na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Majaliwa amechukua uamuzi huo kutokana na idadi kubwa ya watoto wa kike wanaokatisha masomo kutokana na ujauzito.

“Jambo lingine litakalowawezesha kukabiliana na tatizo la ujauzito kwa wanafunzi wa kike ni kuanzisha miradi ya ujenzi wa mabweni ili watoto wa kike waweze kusoma bila ya kupata vishawishi vinavyosababisha wao kupata ujauzito.”

Majaliwa amesema Serikali haiwezi kuacha jambo hilo likiendelea, hivyo aliwataka wananchi washirikiane katika kuwalinda watoto wa kike na Serikali itawachukulia hatua watendaji wote ambao katika maeneo yao watoto wa kike watabainika kuwa na ujauzito.

“Watoto wa kike lazima waheshimiwe waachwe wasome bila ya usumbufu na atakayekatisha masomo adhabu yake ni kali. Tukikukuta umesimama na binti katika kona isiyoeleweka tutakukamata. Ole wenumtakaobainika kuwapa ujauzito wanafunzi, adhabu yake ni miaka 30 jela.”

Ametoa onyo kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto kike ambao bado ni wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto wao wa kiume kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.

Katika kuoneshwa kuchukizwa na jambo hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mwita Waitara ambaye anashughulikia elimu, amemueleza Waziri Mkuu kwamba Novemba 30, 2018 yeye arudi wilayani hapo kwa  ajili ya kuwashughulia wote wanaokatisha masomo wanafunzi kike. Ametoa namba ya simu ili wananchi waanze kumpa taarifa za wahusika.

Mertesacker ampigia debe Arsene Wenger
Sakata la dawa za kulevya laibuka tena, sasa ni zamu ya Zanzibar