Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa bodi ya KADCO uhakikishe unaweka mabango ya kielektroniki yenye kuonyesha vivutio vya utalii kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Ametoa agizo hilo wakati akikagua miundombinu ya uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kuwaaga watalii 274 kutoka Israeli wanaowawakilisha wenzao 1,000 walioondoka nchini jana kurejea kwao.

Akiwa uwanjani hapo, Waziri Mkuu alikagua eneo la mapokezi, sehemu ya abiria wanaoondoka na wanaowasili, sehemu ya uhamiaji, mashine za kukagua mizigo ya wanaoondoka na wanaowasili, sehemu za kutolea huduma na maduka.

“KADCO na Wizara ya Maliasili na Utalii, shirikianeni kuweka utaratibu wa kutangaza vivutio vyetu vya utalii hasa wanyama kwenye viwanja vyote vya ndege, tunazo mbuga, milima, fukwe za bahari na ngoma za makabila mbalimbali, wekeni mabango yanayobadilisha picha, Screens zenye wanyama wanaobadilikabadilika zinaleta mvuto lakini pia ni fursa ya kutangaza vivutio vyetu, nimezunguka humu ndani, kuta zote ni nyeupe tu, tumieni fursa hiyo kutangaza tamaduni zetu na vivutio tulivyonavyo,”amesema Majaliwa

Akiwa uwanjani hapo, Waziri Mkuu alikagua eneo la mapokezi, sehemu ya abiria wanaoondoka na wanaowasili, sehemu ya uhamiaji, mashine za kukagua mizigo ya wanaoondoka na wanaowasili, sehemu za kutolea huduma na maduka.

Pia amemwagiza Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji kwenye kiwanja hicho cha ndege, Filbert Ndege awasiliane na makao makuu yake ili waangalie uwezekano wa kuongeza madirisha ya kutolea huduma za uhamiaji (counters) ili huduma hiyo itolewe kwa kasi zaidi.

 

Prof. Lipumba afanya uteuzi wa wakurugenzi na manaibu wakurugenzi CUF
Video: Rais Magufuli awapa maagizo mazito wakuu wa mikoa, Profesa Chuo Kikuu amgeuzia kibao Dkt. Bashiru