Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Cassim Majaliwa, ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kupitia Jeshi la Polisi kufanya upelelezi  na kuwakamata wote  waliohusika na mauaji ya watu saba ambao miili yao iliokotwa pembezoni mwa mto Ruvu Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Majaliwa amesema kuwa Serikali imepokea kwa huzuni kubwa kwa taarifa ya kuokotwa kwa miili hiyo Desemba 8, mwaka huu na kusema kuwa matukio kama hayo likiwemo la mjasiriamali kutekwa Mkoani Tabora, hayakubaliki wala kuvumilika.

“Serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi tutaendelea na upelelezi ili wahusika wachukuliwe hatua kali ili kukomesha vitendo na mauaji ya kikatili kama haya yasijitokeze tena” amesema Majaliwa.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa, uchunguzi umebaini kuwa miili saba iliyookotwa bagamoyo ni ya wahamiaji haramu.

 

 

Gambo: Rais hajazuia kufanya mikutano hotelini
#HapoKale