Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewataka wadhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kupeleka uthibitisho wa maendeleo ya afya yake siku ambayo kesi hiyo itakapotajwa tena Mahakamani hapo.

Agizo hilo limetolewa leo baada ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba, kuuliza maendeleo ya Lissu na Mdhamini wake, Robert Katula kueleza kuwa Lissu bado anaumwa.

Baada ya maelezo hayo kutoka kwa mdhamini, wakili wa Serikali, Estazia Wilson alieleza kuwa shauri hilo lililo pelekwa kwaajili ya kusikilizwa haliwezi kuendelea hivyo Lissu atasubiriwa hadi pale afya yake itakapo imarika.

Hakimu Simba akaahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21, 2019.

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu anakabiliwa na mashtaka matano, likiwemo la kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria.

Mahakama ya Rufani yathibitisha umri wa kuolewa
Video: INAUMIZA! Baada ya kukatwa Ulimi, Saratani yatoboa Shingo | Chakula kinatoka| Mkewe aomba msaada