Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AFCHPR), imeendelea kufuatilia kesi iliyokuwa inawakabili wasanii wa muziki wa dansi nchini, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mtoto wake Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha baada ya kuwekwa hatiani kwa makosa ya ubakaji na ulawiti.

Akiendesha mashtaka hayo Jaji, Niyungeko ambaye ni raia wa Burundi, amedai kuwa Mahakama ya Tanzania katika mwenendo mzima wa kesi hiyo kwa upande mmoja iliwatendea haki washtakiwa lakini kwa upande mwingine haikuwatendea haki kutokana na kwamba watuhumiwa hawakupata nafasi nzuri ya kujitetea wakati wa mwenendo wa kesi.

Ambapo kufuatia kesi hiyo, wasanii hao walikata dhamana ya kupinga hukumu ya kifungo cha maisha jela.

Hivyo waliwasilisha hoja mbalimbali mahakamani zikiwemo hoja zilizokubaliwa lakini pia kulikuwa na hoja ambazo zilikataliwa na mahakama.

Hoja zilizokubaliwa na mahakama ni pamoja na Mtuhumiwa Nguza Viking kutokukubaliwa kupimwa nguvu za kiume baada ya kudai kuwa hana nguvu za kiume, katika kuthibitishia mahakama kuwa asingeweza kufanya kosa aliloshitakiwa nalo.

Lakini pia hoja nyingine ni kwamba watuhumiwa hawakupata fursa ya kuwauliza maswali waliotoa ushahidi ili kuthibitisha makosa yao.

Hoja ya tatu watuhumiwa hawakupata maelezo ya mashahidi.

Pamoja na hoja hizo zilikubaliwa zipo hoja ambazo mahakama ilizitupa kapuni, ikiwemo.

Watuhumiwa waliomba kutolewa magereza, lakini kwa sasa jambo hilo tayari limekamilika kufuatia msamaha wa rais, alioutoa Disemba 9, mwaka jana katika maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru yaliyofanyika jijini Dodoma.

 

 

Serikali yapewa mwezi mmoja kujibu fidia kesi ya Babu Seya na mwanae
Video: Kampuni ya DataVision International kufanya mambo makubwa mwaka 2018