Baada ya juzi Rais John Magufuli kumlipia mbunge Peter Msigwa faini ya sh. 38 milioni kati ya sh. 40 milioni alizotakiwa kulipa mbunge huyo ili atoke jela baada ya familia yake kuchangia milioni 2, malipo hayo yaliibua mjadala baada ya Chadema kutoa taarifa kuwa nao wamelipa faini hiyo.

Utata ulioibuka ni watu kuhoji ilikuwaje mbunge huyo akalipiwa faini mbili tofauti, wakati namba ya malipo ya pesa hizo kutoka mahakamani kwa kawaida huwa ni moja tu kwa kila mtu anayetaka kufanya malipo.

Mahakama ya kisutu imetoa ufafanuzi wa mkanganyiko huo, ikibainisha kuwa malipo yaliyoanza kuwasilishwa mahakamani hapo ni ya Rais Magufuli.

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Kisutu, Godfrey Isaya ameiambia Mwananchi kuwa namba ya malipo ya faini ya mtu aliyehukumiwa kulipa faini huweza kutolewa kwa watu  zaidi ya mmoja na hilo si tatizo.

Amesema namba ya malipo inakubali malipo kama kawaida na huingia katika mfumo ambao unaweza kutambulika na hata kama mtu akifanya kosa lingine akahukumiwa, akilipa faini atapewa ‘control’ namba hiyo hiyo kulipia.

” Kwahiyo malipo yaliyoingia kwanza kwenye ‘system’ ni ya Rais Magufuli na sisi hayo ndiyo tuliyapokea na kuyaidhinisha” amesema hakimu Isaya.

Amebainisha kuwa kutokana na hali hiyo, uongozi wa Chadema uliwasilisha maombi mahakamani hapo ili malipo waliyolipa kwa mchungaji Msigwa yahamishiwe kwa Heche, na mahakama ilikubali.

Jeshi la Magereza lakanusha kauli za viongozi wa CHADEMA
Corona Kenya: Sabuni za mikono zaadimika