Rais dkt. John Magufuli amempongeza Prof. PLO Lumumba kwa juhudi zake za kueleza waziwazi makosa yanayosababisha nchi za Afrika kubaki nyuma kiuchumi, kijamii na kisiasa, wajibu wa viongozi na wananchi wa Afrika katika kukabiliana na changamoto zinazozikabili nchi zao na mapenzi yake makubwa kwa Afrika.

Rais Magufuli amemueleza juhudi ambazo Serikali ya Awamu ya tano inazifanya katika kujenga uchumi imara wa kujitegemea ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge railway-SGR), ujenzi wa Bwawa la Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 za umeme, kuongeza usambazaji wa umeme kutoka vijiji 2,018 hadi kufikia vijiji 8,587.

Ujenzi wa barabara na madaraja makubwa na madogo, kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari, kuongeza mikopo ya elimu ya juu, kuongeza ukusanyaji wa mapato, kudhibiti rasilimali muhimu ya madini na kupambana na rushwa.

“Mimi sijawahi kukutana nawe kabla, lakini nakusikia na kukuona kupitia vyombo vya habari jinsi unavyopaza sauti kuhusu Bara la Afrika, nakupongeza kwa juhudi hizo, na ninafarijika kwamba unaisemea vizuri Afrika” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Prof. PLO Lumumba, raia wa Kenya, amemshukuru Magufuli kwa kutenga muda wake kuzungumza naye, na amempongeza kwa juhudi kubwa alizozionesha katika kipindi kifupi cha uongozi wake wa miaka 4 ambapo ameonesha mfano wa kuigwa na nchi nyingine za Afrika.

kupigania rasilimali za nchi ikiwemo madini, kujenga nidhamu ya utumishi Serikalini, kuimarisha uchumi, kupambana na wizi wa mali za umma, rushwa na ufisadi.

China: Maambukizi ya Corona yapungua kwa asilimia 80
Togo: Faure ashinda kwa kishindo urais

Comments

comments