Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametoa tahadhari kwa wananchi juu ya kujikinga na ungonjwa uliotangazwa kuwa janga la dunia na shirika la afya duniani (WHO), virusi vya Corona ambavyo bado havijaingia nchini.

Akizungumza leo Machi 13, 2020 wakati akizindua karakana kuu ya jeshi la wananchi JWTZ jijini dar es salaam, iliyokamilishwa kwa msaada wa serikali ya Ujerumani kwa gharama ya shilingi bilioni 8.5.

Rais Magufuli amesema licha ya kuwa virusi vya Corona bado havijaingia nchini, lakini tanzania haiwezi ikajiweka pembeni, tayari waziri wa afya ameshatoa muongozo wa jinsi ya kujikinga ambao unatakiwa kuzingatiwa na wananchi wote.

” Ndugu zangu watanzania tusipuuze ugonjwa huu.., kwa wale wanaopenda kusafiri kama safari sio ya lazima sana usisafiri, na nimeshatoa maagizo hatutatoa vibali vya watu kusafiri tu wanavyotaka.., hata kwa watanzania wenye mazoea ya kusafiri umefika wakati wakuji ‘limit’ katika safari zetu kwaajili ya kujilinda na tatizo hili” .

Katika hatua ya kuchukua tahadhari ametoa agizo kuwa wasiachiwe viongozi pekee wazungumze, tahadhari ianze kutolewa kwa ngazi ya familia, shuleni walimu watoe tahadhari kwa wanafunzi na watoto, pamoja na kwenye usafiri wa magari ya umma.

“Hii tahadhari msiwaachie tu viongozi.., mashuleni walimu watoe tahadhari kwa wanafunzi na watoto, kwenye vyuo vyetu, kwenye majeshi, makambini, kwenye magari, ikiwenzekana hata kwenye daladala kondakta atoe angalau hata elimu kidogo”

Adha amesisitiza kujifunza kwenye maandiko ya zamani juu ya kufuata tahadhari zinazotolewa kama ilivyo kuwa wakati wa sodoma na gomola pamoja na wakati wa kuchonga safina ya nuhu.

Jamhuri yapinga maombi ya Rugemalira kuachiwa na Mahakama
Mnyika na wenzake wachomoka Segerea, Mbowe abaki pekeyake