Wakati Tanzania inaonekana kuwa katika kilele cha changamoto ya vyama vingi vya siasa vinavyotoa ahadi mbalimbali kwa wananchi ili vipate idhini ya wananchi kuunda serikali, mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amesema nchi hii haihitaji vyama vya siasa bali inahitaji mtatuzi wa matatizo.

Dk. Magufuli aliyasema hayo wakati alipokuwa akihutumia umati mkubwa wa wananchi katika kijiji cha Mlangali, Ludewa ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kampeni nchini. Alisema vyama vingi vya siasa vilivyopo hivi sasa havitakuwepo endapo watanzania watatuliwa shida zao.

“Watanzania hawahitaji vyama, ukitatua matatizo yao tu hata Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi havitakuwepo,” alisema Magufuli.

Aliwataka wananchi kumchagua yeye kwa kuwa atakapoingia madarakani atahakikisha anaijenga Tanzania mpya na atakuwa rais wa watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama, makabila au hata dini zao.

Mgombea huyo anaendelea kuzunguka katika maeneo mbalimbali nchini akinadi ilani ya CCM huku akitoa ahadi mbalimbali katika maeneo anayopita.

Dk. Slaa Kupasua Jipu Leo, Kubadilisha Hali Ya Kampeni
Lowassa ‘Avuta Pumzi Ya Mwisho’ Kuiondoa CCM