Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli amewahidi kushughulikia tatizo la masoko katika kilimo cha tumbaku ili kuwanufaisha zaidi wakulima.

Mgombea huyo ametoa ahadi hiyo jana mkoani Tabora katika mkutano wa Kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mkoa huo waliofika kusikiliza sera za CCM.

Aliwahakikishia wakulima hao kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa rais, suala la kwanza litakuwa kuwahakikishia wakulima soko la tumbaku pamoja na bei bora ya zao hilo.

“Serikali ya Magufuli, itakapowekwa madarakani, kazi ya kwanza itakuwa kusimamia bei ya tumbaku,” alisema.

Dk Magufuli pia aliwaahidi wananchi wa mkoa huo kuwa kazi ya kujenga barabara inaendelea na ataikamilisha kwa kiwango kikubwa atakapokuwa madarakani.

Wakazi wa Kaliua, Tabora wakimsikiliza Dk Magufuli

Wakazi wa Kaliua, Tabora wakimsikiliza Dk Magufuli

“Tunatengeneza barabara ya kutoka Nzega hadi Tabora, Kilometa 116, tunatengeneza kutoka Tabora kwenda Urambo, tunatakiwa tutengeze ya kutoka Urambo kwenda Kariua, lakini kutoka Kariua kwenda Kasirambwa, kutoka Kasirambwa kwenda Maragarasi, Maragarasi kwenda Kigoma, na tukifika Kigoma tuitandike iende mpaka Nyakanazi,” alisema Dk Magufuli.

Mgombea huyo alimaliza ziara yake Mkoani Tabora ambapo leo anatarajia kuanza kampeni zake mkoani Kigoma.

 

Nape aahidi Kuimulika Mtama Nzima
Klabu Za Ligi Kuu Kuendeleza Mchakato Kesho