Baada ya kipenga cha NEC kupulizwa rasmi kwa wagombea kuchukua fomu za kuwania urais wa Tanzania, leo majira ya saa sita mchana mgombea wa CCM, Dk. John Magufuli anatarajia kuchukua fomu.

Tukio hilo la kuchukua fomu ya urais linatarajiwa kuambatana na msafara mrefu wa wana chama wa CCM wanaomuunga mkono mgombea huyo ili kuonesha jinsi anavyokubalika.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye ametaja barabara ambazo bila shaka zitalazimika kufungwa kwa muda wakati msafara wa Dk. Magufuli unapita.

“Msafara utaanza saa tano asubuhi na tunategemea utafika tume ya uchaguzi saa sita mchana. Msafara huo utapitia barabara ya Morogoro, barabara ya BibiTiti na barabara ya Ohio na utarudi kwa njia hiyo hiyo,” alisema Nape.

Hata hivyo, Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi (NEC) ilitoa katazo kwa wagombea kuchukua fomu kwa utulivu bila mbwembwe.

Nape Awafananisha ‘Akina Lowassa’ Na Oil Chafu
Rapa wa Kike Amvaa Nicki Minaj