Rais Dkt. John Magufuli amesema shughuli za serikali za nchini Tanzania zitaendelea kufanyika vikiwepo vikao vya madiwani, vikao vya Bunge pamoja na uchaguzi mkuu ujao licha ya mlipuko wa virusi vya covid 19.

Amebainisha hayo leo Machi 26, 2020, alipokuwa akipokea ripoti kutoka kwa mkaguzi mkuu wa Serikali CAG, Charles Kichere na ripoti kutoka ofisi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru, Ikulu, Chamwino jijini Dodoma.

Rais Magufuli amesema ameshangazwa kuona moja ya gazeti hapa nchini limeandika vikao vya madiwani vimefanyika licha ya mlipuko wa corona kwani shughuli za serikali hazijazuiliwa na kazi lazima ziendelee kufanyika.

” Kazi lazima iendelee kufanyika na uchaguzi tutafanya tu, wapo wengine wanafikiri nitaahirisha, nani anataka akae kwenye maofisi haya muda wote huo” Amesisitiza rais Magufuli…, Bofya hapa kutazama.

CAG abaini mapungufu CUF na CCM, fedha za ruzuku zatajwa
Boti zatumika kusafirisha wananchi wa Rufiji