Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli leo tarehe 10 Julai,2020 amemteua Gabriel Pascal Malata kuwa wakili Mkuu wa Serikali (solicitor General).

Kabla ya uteuzi huo, Malata alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na anachukua nafasi ya Dkt. Julius Clement Mashamba.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Boniface Luhende kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Deputy solicitor General).

Kabla ya uteuzi huo, Dkt.Luhende alikuwa Mhadhiri katika shule kuu ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na anachukua nafasi ya Malata ambaye ameteuliwa kuwa wakili Mkuu wa Serikali.

Vandenbroeck: Wasubiri makali na hasira za kikosi changu
JPM ateua Mkuu wa wilaya Nzega