Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli amewatahadharisha watanzania kutokubali kufanya mabadiliko kwa haraka kwa kuwa mabadiliko hayo yanaweza kusababisha machafuko.

Akiongea leo katika mkutano wa kampeni mjini Musoma, Dk Magufuli ametoa mfano wa machafuko yaliyojitokeza nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 akidai yalitokana na hatua za harakaharaka.

Amewataka wananchi wa Musoma kumchagua yeye kwa kuwa anataka kuwa rais wa amani na rais wa watanzania wote anaechapa kazi bila kujali vyama vyao vya siasa wala kabila.

Kadhalika, Dk Magufuli amewaondoa wananchi na wafanyakazi wanaodhani kuwa yeye ni mkali sana.

“Wengine wanasema lakini huyu Magufuli ‘mbona mkali sana’, jamani mimi ni mpole mno, lakini kwa mafisadi ntakuwa mkali sana,” alisema huku akishangiliwa na wananchi.

Mgombea huyo aliwaahidi mabadiliko wananchi wa Musoma endapo watakamchagua kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano huku akiwaahidi kuondoa kabisa tatizo la maji, miundombinu na kufuta michango na karo za wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

Aidha, aliisisitiza ahadi ya chama chake kuwa watatoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na kila kata kwa ajili ya kukopesha vikundi mbalimbali kwa lengo la kuwakwamuwa wananchi kiuchumi.

Siri 5 kubwa Za Mafanikio Bila Utegemezi
Waangalizi Wa Uchaguzi Wa Kimataifa Watahadharishwa