Rais Dkt. John Magufuli, ameagiza wakazi wa kijiji cha Nanyala wilayani Mbozi mkoani Songwe, kuendelea kulitumia eneo lenye ukubwa wa Ekari 2,115 linalo gombaniwa baina ya wakazi hao na kiwanda cha saruji Mbeya.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo aliposimama katika kijiji hicho katika ziara yake mkoani Songwe na kuelezwa kero hiyo na mwenyekiti wa kijiji, Philemon Namwema.

Katika maelezo yake, Namwema amesema kuwa mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na wamezuiwa kufanya shughuli yeyote huku wananchi wengine 23 wakikabiliwa na kesi mahakamani.

Akitoa uamuzi huo, Rais Magufuli amewaagiza Mawaziri husika kukaa pamoja na kufuta kesi iliyopo mahakamani na baada ya hapo wamjulishe ili aweze kubadili matumizi ya ardhi katika eneo hilo.

Miraji Athumani ampiku Meddie Kagere VPL
Ngorongoro Heroes kuikabili Kenya kesho