Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Juma Malewa amesema kuwa msamaha uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Uhuru Desemba 9, 2017 haukumhusu msaani wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu.

Amefafanua kuwa mchakato wa kuanza kuangalia wafungwa wakupunguziwa vifungo na kusamehewa haukumhusisha msanii huyo.

Amesema kuwa vipo vigezo vingi vinavyoweza kumfanya mfungwa asamehewe ama kupunguziwa kifungo kutokana na kosa na muda wa kifungo chake na kwamba misamaha inatofautiana kutokana na kosa.

“Msamaha huu haukumuhusu yeye kwa sababu aliingia magereza wakati tayari zoezi hili lilikuwa limekamilika,”amesema Malewa

Hata hivyo, Desemba 9 mwaka huu siku ya Uhuru kwa mujibu ya ibara ya 45 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli alitoa msamaha kwa  wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya ) na Johnson Nguza (Papii Kocha ) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela na wengine kupunguziwa vifungo vyao

 

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 14, 2017
Yanga, Simba kuanzia ugenini michuano ya kimataifa