Wapiganaji wenye uhusiano na kundi la kigaidi linalojiita Islamic State (IS) wamepandisha bendera zao kwenye mji wa Baga nchini Nigeria baada ya kuudhibiti.

Kwa mujibu wa BBC, mamia ya wakaazi wa mji huo wameukimbia kufuatia mapigano kati ya jeshi la Serikali na magaidi hao Jumatano wiki hii.

Imeelezwa kuwa wapiganaji hao waliteka silaha kutoka kwenye kambi ya jeshi pamoja na eneo la kijeshi la ufukwe wa Lake Chad.

Hata hivyo, jeshi la Serikali limekanusha kushindwa katika mapigano hayo na kueleza kuwa wamefanikiwa kuurejesha mji huo. Lakini, PRNigeria, chombo cha habari chenye uhusiano wa karibu na jeshi kimemkriri afisa wa intelijensia ya jeshi hilo akieleza kuwa wameamua kuondoka kama mbinu ya kiufundi ya kupanga mashambulizi ya kuurejesha mji huo.

“Jeshi la Nigeria limejipanga na limerusha ndege zake za kivita Jumatano usiku hadi Alhamisi baada ya kujiondoa kwanza kwenye mji huo kama mbinu ya kujipanga,” PRNigeria imemkariri afisa huyo.

Wakaazi wa mji huo ambao walifanya mazungumgumzo na BBC, wanaeleza kuwa wanajeshi wa kundi hilo la kigaidi wameonekana kwenye maeneo ya mji huo na kwamba baadhi yao walishiriki sala ya jioni na wananchi wa mji huo.

Wameeleza kuwa wapiganaji hao waliwaahidi wananchi kuwa hawatawashambulia kwani sio walengwa na kuwaruhusu kuondoka katika mji huo.

Wapiganaji hao wanajitambulisha kama Islamic State’s West Africa Province (Iswap), ambao wanaungwa mkono na kundi la IS ambalo hivi karibuni lilitangaza kujitenga na Boko Haram.

Kanyasu atoa maagizo mazito wilayani Buchosa
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 29, 2018