Kaya 59 wilayani Sengerema mkoani Mwanza zimekosa makazi ya kuishi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jumamosi.

Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amebainisha kuwa baada ya tathimini kufanywa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya imebaini kaya 59 zimekosa makazi na watu 100 hawana chakula na mahitaji mengine baada ya vitu vyao kusombwa na maji.

Amewaomba wadau mbalimbali kujitolea kuwahifadhi watu hao na kutoa michango ya chakula, dawa pamoja na vitu vingine ili kuwasaidia waathirika hao.

Amesema tayari kamati ya ulinzi na usalama imeweka utaratibu wa kupokea misaada ambapo ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Sengerema pamoja na ofisi ya katibu tawala wataratibu shughuli ya kupokea michango.

“Tunawaomba watu na taasisi mbalimbali kujitokeza kutoa misaada lengo ni kuwasaidia watu hawa waliokubwa na mafuriko tuweze kuwasaidia ” amesema kipole.

Aidha Mbunge wa Sengerema (CCM), Wiliamu Ngereja anafanya ziara ya siku moja ya kuwatembelea watu waliokubwa na mafuriko kisha kutoa mkono wa pole kwa waliopoteza ndugu zao.

Arsena kumkosa Xhaka, Modric kutua Inter
LIVE Dodoma: Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi, ujenzi wa makao Makuu ya ulinzi wa Taifa