Maelfu ya wananchi nchini Morocco wameandamana katika mji wa Rabat wakitaka serikali iwaachilie huru wanaharakati ambao waliongoza maandamano ya kulalamikia matatizo ya kiuchumi na kijamii katika eneo la Rif Kaskazini mwishoni mwa mwaka 2016 na 2017.

Wiki mbili zilizopita Mahakama ya Rufaa mjini Casablanca iliidhinisha kifungo cha miaka 20 gerezani kwa wanaharakati hao ambao ni Nasser Zefzafi, Nabil Ahamjik, Ouassim Boustati na Samir Ighid waliopatikana na hatia ya kuvuruga nidhamu ya umma na kuwa tishio kwa umoja wa kitaifa.

Wanaharakati wengine 35 walihukumiwa vifungo vya kati ya miaka miwili hadi 15 jela. huku wakiwa wamebeba bendera za jamii ya Amazigh, na picha za wanaharakati waliofungwa jela walitoa ujumbe kama vile uhuru, heshima na uadilifu wa kijamii.

Aidha, maandamano hayo yamezileta pamoja familia za wanaharakati hao wa eneo la Rif, mashirika ya kutetea haki za binadamu, harakati ya Amazigh, vyama vya mrengo wa kushoto na harakati ya Kiislamu zilizopigwa marufuku zijulikanazo kama Al Adl-wal-Ihsan.

Maandamano ya Rif na yale ya mji wenye migodi wa Jerada yametajwa kuwa mabaya zaidi nchini humo tokea mwaka 2011 na yalimfanya Mfalme Mohammad wa Sita kujipunguzia mamlaka yake na kuyakabidhi kwa bunge.

Hata hivyo, maandamano hayo yalianza mwezi October 2016 baada ya mjasiliamali mmoja masikini wa biashara ya samaki katika jimbo la BerBer Rif kugongwa na kufa wakati akijaribu kumuokota samaki wake aliyechukuliwa na polisi na kutupwa kwenye lori la takataka.

Video: Hakuna Alikiba bila Diamond wala Diamond bila Alikiba, tazama ngoma zao hapa chini
Wananchi wa Mtulingala wajenga Zahanati ya Kijiji

Comments

comments