Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amesema kuwa hakuna haja yakutumia zaidi ya milioni mia saba kwa ajili ya kufanya marudio ya uchaguzi wa udiwani wa kata tatu baada ya madiwani wa CHADEMA kudaiwa kununuliwa na CCM.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Machame Uroki akiwa kwenye ziara yake jimboni Hai.

Aidha, amesema kuwa fedha ambazo zinakwenda kwa ajili ya uchaguzi wa marudio zingeweza kufanya mambo mengine ya msingi lakini si marudio ya uchaguzi wa kata hizo.

“Gharama ya kurudia uchaguzi wa diwani mmoja ni shilingi milioni mia mbili hamsini, madiwani watatu waliopewa fedha wakaikimbia CHADEMA wakawaacha wananchi huo ni usaliti gharama ya kurudia uchaguzi kwenye kata tatu ni milioni mia saba na hamsini,”amesema Mbowe

Hata hivyo, ameongeza kuwa licha ya madiwani hao kununuliwa hata uchaguzi ukifanyika kesho anaamini kuwa chama chake kitaibuka na ushindi kwa kata zote tatu

LIVE: Yanayojiri uchaguzi mkuu wa TFF Dodoma
Video: Lowassa achekelea, Waziri akwepa kutumbuliwa

Comments

comments