Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa amepokea kwa masikitiko ajali ya moto iliyotokea leo Mei 23, 2019, kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ashira iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.

Mghwira amesema kuwa bado hajapata tathmini kamili ya ajali, lakini Kamanda wa Polisi mkoani humo ambaye amewahi eneo la tukio, amemweleza kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa hakukuwa na mwanafunzi bwenini.

”Shule ya Ashira ni miongoni mwa shule kongwe ambazo zipo kwenye mpango wa kufanyiwa marekebisho na niliitembelea hivi karibuni, lakini nasikitika leo imeungua upande wa mabweni. baadaye tutapata tathmini maana Kamanda yupo kule na RAS naye amekwenda,”amesema Mghwira

Mapema leo Mei 23, 2019, majira ya saa 6:00 mchana ulizuka moto shuleni hapo na kuunguza mabweni ya wanafunzi.

 

Waziri Kalemani awataka wananchi kutunza miundo mbinu ya Umeme
Cardi B amehairisha tamasha kisa upasuaji

Comments

comments