Rapa Mabeste ambaye hivi karibuni yeye na aliyekuwa mke wake, Lisa wamekuwa sehemu ya gumzo kwenye vyombo vya habari baada ya kujitokeza na kuzungumzia chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yao mwaka mmoja uliopita, ametoa mtazamo wake kuhusu uamuzi wa Stamina kuachia ‘Usiwaze’.

Wiki mbili zilizopita, Stamina alikuwa gumzo kila kona baada ya kuachia wimbo huo ambao ulianika mengi aliyoeleza kuwa ni chanzo cha kuachana na mkewe, akidai kuwa mkewe alimsaliti hadi kufikia hatua ya kujutia hata muda aliotumia kufunga ndoa kanisani.

Mabeste ambaye hivi karibuni yeye ameachia wimbo unaoitwa ‘Qualify’, ameeleza kuwa yeye pia wakati akiwa na uchungu wa kuvunjika kwa ndoa yake aliandika na kurekodi nyimbo nane zikieleza jinsi alivyoyachukia mapenzi, lakini baada ya kutafakari aliona sio busara kuziachia.

“Mama Kendrick aliponiambia tuachane, kwakweli nilipokuwa naenda studio… nina albam ya nyimbo za kuchukia mapenzi, lakini sasa bado nafanya lakini kuna roho inaniambia ‘sio mimi huyu’, producer anazimix na anasema ni kali, lakini kila akisubiri nitoe nawaza ‘kweli mimi mapenzi yanidrive kiasi hiki…hapana’,” alisimulia Mabeste.

Rapa huyo wa ‘Baadaye Sana’ ameeleza kuwa aliamua kuziacha kabisa nyimbo hizo na kwamba ataendelea kufanya kile ambacho anakifanya siku zote.

Ametoa ushauri kwa watu wanaoingia kwenye ndoa kuwa wanapaswa kuwa na kifua cha kuvumilia na kujiandaa kisaikolojia kuwa huenda siku moja mambo yanaweza kwenda tofauti nawalivyotarajia.

“Unapokuwa na mwanamke, ukaishi naye, basi jiandae endapo kuna jambo litatokea, jiandae kwamba likitokea tatizo nitakubaliana nalo vipi kwa sababu na yeye ni binadamu, sio malaika,” ameongeza.

Mabeste ameeleza kuwa yeye anaona ni vyema zaidi kuwa na vifua vya kutunza yanayoendelea kwenye masuala ya uhusiano.

Amesema kuwa kwa alichokifanya Stamina hana budi kumuunga mkono kwa sababu mwenyewe aliyeona ni sawa lakini kwa upande wake ameshindwa kuzitoa nyimbo kama hizo kwa sababu aliona ni busara kumstahi mama watoto wake kwakuwa wimbo unaishi milele na watoto wangekuja kuusikiliza pia.

Zijue faida za vitamini A mwilini
Maeneo matatu muhimu ya kuweka 'Dustbin' ndani ya nyumba

Comments

comments