Udart kupitia Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, Deus Bugaywa ametoa taarifa ya kusitisha huduma ya mabasi yaendayo kasi na kusema kwamba kampuni hiyo itatoa huduma kwa safari za Kimara-Mbezi na Kimara-Magomeni Mapiga, Gerezani-Muhimbili na Kivukoni Muhimbili.

Hivyo imesitisha huduma zake kati ya Kimara – Kivukoni, Kimara – Gerezani, Morroco – Kivukoni na Morroco – Gerezani kuanzia saa 10: 30 alfajiri leo Jumatatu Mei 13, 2019.

Hatua hiyo ni kufuatia kujaa maji katika eneo la Jangwani.

Aidha ufuatiliaji unaendelea kuona hali ya maji katika eneo husika, ambapo kama maji yakipungua huduma zitarejea katika hali ya kawaida.

Wameomba radhi kwa usumbufu kutokana na kusitishwa kwa safari hizo.

Hata hivyo barabara ya Kinondoni kwenda Magomeni imefungwa, Magari yote hayapiti kutokana na bonde la Mkwajuni kujaa maji.

Pia mabasi ya kwenda Kilimanjaro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Songea, Kigoma, Mpanda, Kagera, Morogoro na maeneo mengine yamebadilisha njia na kwamba, yanatoka Ubungo kwenda Mwenge, kisha Tankibovu na kuchukua Barabara ya Goba kwenda hadi Mbezi na kisha kuendelea na safari.

Kodak Black afungwa jela ya kijasusi
Video: Baba auza mtoto kwa milioni 5, Mapendekezo saba ya Chadema