Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka DART, inautaarifu umma kuwa leo, Jumatano ya Aprili 10 kutakuwa na uhaba wa mabasi katika mfumo wa DART.

Hii inatokana na baadhi ya mabasi kuwa na hitilafu zinazohitaji matengenezo makubwa na madogo.

Ambapo kati ya mabasi 82 ambayo yanafanya kazi katika mfumo wa DART, mabasi 58 yameondoloewa barabarani kufanya kazi kwa ajili ya matengenezo.

Taarifa hiyo imetolewa na Meneja Uhusiano kwa Umma wa DART, William Gatambi.

 

 

LIVE: Rais Magufuli akizindua ujenzi wa barabara Njombe - Moronga
Video: Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi Tanzania watinga Dodoma

Comments

comments